National Curriculum and Development Center NCDC
LOWER SECONDARY CURRICULUM
LUGHA YA KISWAHILI
TEXTBOOK
LOWER SECONDARY CURRICULUM
LUGHA YA KISWAHILI
TEXTBOOK
Mwanafunzi mpendwa, kitabu hiki kimeandikwa kukidhi matakwa ya mtaala mpya wa sekondari wa
kidato cha kwanza hadi cha nne uliofanyiwa marekebisho na Kituo cha Taifa cha Kuendeleza Mitalaa.
Mtalaa huu unalenga mwanafunzi kwa kumshirikisha katika shughuli za mafunzo mbalimbali.
Unalenga kujenga na kukuza mwanafunzi atakayekuwa na milisi zinazohitajika katika karne ya 21.
Kitabu hiki kinalenga kidato cha kwanza na kina mada tisa. Mada hizi zimeandikwa zikilenga kukuza
milisi za wanafunzi kutokana na matarajio lengwa ya kila mada. Shughuli za Mafunzo zimependekezwa zenye lengo la kukuza stadi za kimaisha kama vile kutafakari, ubunifi, mawasiliano
bora, utatuzi wa changamoto mbalimbali, ushirikiano, pamoja na matumizi ya TEHAMA. Maadili pia
yamekuzwa katika shughuli hizi. Mtalaa unakisi Maisha ya kawaida yanayopatikana katika mazingira